Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya Alphonso Davies yapamba moto Ulaya

Alphonso Davies Bn Vita ya Alphonso Davies yapamba moto Ulaya

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wanaripotiwa kuwa wanapambana kumbakiza beki Alphonso Davies kwani Real Madrid imepanga kumbeba mwakani.

Nyota huyo wa Canada mwenye umri wa miaka 22, yupo chini ya mkataba na mabingwa hao wa Bundesliga hadi Juní 2025.

Mazungumzo kuhusu mkataba mpya yameanza, lakini uvumi unaongezeka kwamba majadiliano hayo yamekwama.

Gazeti la Bild linaeleza kwamba Real Madrid inatarajiwa kutuma Pauni 35 Milioni kwa ajili ya kumnunua beki huyo mwisho wa msimu.

Chapisho la gazeti hilo kutoka Ujerumani limeandika kwamba: “sio siri tena, Real Madrid inahitaji saini ya Davies atakapoingia miezi 12 ya mwisho ya mkataba.”

Davies aliondoka Vancouver Whitecaps kwa ajili ya kujiunga na Bayern Munich 2019, na tangu hapo beki huyo amekuwa mmoja wa vipaji vinavyowindwa Ulaya akisaidía Bayern kubeba mataji matano likiwemo la Ligi ya Mabingwa ilipobeba 2020.

Jude Bellingham amekiwasha Ligi Kuu Hispania tangu aliponunuliwa kutoka Borussia Dortmund na Bild linaripoti Madrid inataka kuongeza kifaa kingine kama sehemu ya kuboresha kikosi.

Pia bado ina nia ya kumnunua nyota wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe na inaonekana kuwa tayari kumpata mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa msimu ujao.

Vile vile Los Blancos inahusishwa na kiungo anayekipiga Newcastle United, Bruno Guimaraes.

Hata hivyo hivi majuzi alikubali kusaini mkataba mpya hadi 2028 na amewekewa kifungu cha kununuliwa kwa Pauni 100 milioni kwenye mkataba.

Wakala wa Davies, Nick Huoseh, hivi majuzi alizungumzia tetesi za uhamisho wa kwenda Real Madrid na hakuficha kuzima uvumi huo.

Wakala huyo alisema: “Real ni klabu kubwa. Mimi ni shabiki mkubwa. Kweli Madrid ina jina kubwa. Unaposikia uvumi kuhusu mteja wako akihusishwa inakupa kiburi. Bado tuna mkataba wa miaka miwili Bayern. Tutasubiri kuona jinsi mambo yatakavyokuwa wiki zijazo.”

Chanzo: Dar24