Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita nzito kuibuka usajili wa Harry Kane

Harry Kane.jpeg Harry Kane

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Klabu ya Manchester United huenda ikatibuliwa na Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich kwenye mpango wao wa kunasa saini ya Mshambuliaji Harry Kane kama itaamua kuwa siriazi kwenye msako wa supastaa huyo wa kimataifa wa England.

Bayern wameamua kupoza mpango wao wa kumsajili Kane, kitu ambacho Man United wanajipa matumaini watashinda vita hiyo na kulegeza jitihada zao za kwenda kunasa saini za wakali wengine wawili.

Kane anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake huko Tottenham Hotspur, hivyo huenda wakaamua kumuuza kwenye dirisha hili ili kuhofia kumpoteza bure mwakani.

Hata hivyo, kinachowapa wasiwasi Man United ni kama mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, atakubali kumruhusu Kane kwenda kukipiga Old Trafford msimu ujao.

Na kwenye hilo, endapo kama FC Bayern Munich wataonyesha nia na kuwa siriazi kwenye kumsajili Kane, basi Levy atafanya nao biashara kwa haraka.

Kutokana na hilo ndio maana Man United haijaacha kuzungumza na mastraika wengine kama Victor Osimhen na Randal Kolo Muani kuwaweka kwenye hesabu zao endapo watashindwa kunasa saini ya Kane.

Bayern nayo inaripotiwa kuhitaji huduma ya mastraika hao wengine wawili, Osimhen na Kolo Muani.

Ripoti zinadai Eintracht Frankfurt inamuuza Kolo Muani kwa Pauni 85.8 milioni, huku rais wa SSC Napoli, Aurelio De Laurentiis, naye akiweka wazi Osimhen hawezi kupatikana kwa pesa ndogo.

Washambuliaji wote hao, bei zao zimechangamka akiwamo Kane, ambaye klabu yake ya Spurs inahitaji dau lisilopungua Pauni 100 milioni.

Chanzo: Dar24