Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita msimu ujao Championship ngumu

Mbeya City Kushuka Mbeya City itashiriki Championship msimu ujao

Thu, 29 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mambo yatakuwaje pale msimu wa mwaka 2023/24 wa Ligi ya Championship utakapoanza huku timu mbili pekee ndio zitakazokuwa na nafasi ya kupanda Ligi Kuu.

Utamu wa Championship umenoga zaidi baada ya kushuhudia timu tatu za Ligi Kuu zikishuka daraja kwenda Championship ambazo ni Mbeya City iliyotolewa hatua ya mtoano na Mashujaa.

Timu nyingine ni Polisi Tanzania na Ruvu Shooting huku kutoka First League zikipanda timu tatu kwenda Championship ambazo ni TMA Stars, Cosmopolitan na Stand United.

Msimu ujao tutashuhudia timu sita za majeshi zikiwa Championship ambazo ni Polisi Tanzania, Ruvu Shooting, Mbuni FC, Transit Camp, Green Warriors na TMA Stars.

Jiji la Mbeya kutakuwa na wawakilishi watatu ambao ni Mbeya City, Mbeya Kwanza na KenGold ambazo ziliuhama Uwanja wa Sokoine ambapo KenGold walikuwa wakitumia Uwanja wa Nelson Madela, Sumbawanga, Mbeya Kwanza Uwanja wa Majimaji, Songea. Hata hivyo, vita itanoga hapa zaidi.

MBEYA CITY

Imedumu kwenye Ligi Kuu misimu 10 baada ya kupanda msimu wa mwaka 2013/14 chini ya Juma Mwambusi na kufanya mabo makubwa kwenye soka la bongo ambapo msimu wa kwanza ilimaliza nafasi ya tatu na msimu wa pili ikamaliza nafasi ya nne.

Msimu wa mwaka 2019/20 ilinusurika kushuka daraja wakati timu nne zikishuka ambazo ni Singida United, Ndanda, Lipuli na Alliance wakati Mbao ikishuka kupitia changamoto ya hatua ya mtoano dhidi ya Ihefu FC.

Msimu huo Mbeya City ilikutana na Geita Gold hatua ya mtoano na kutoka suluhu ugenini kisha nyumbani ikashinda 1-0 na msimu huu mambo yamemwendea tena kombo hadi kushuka daraja hivyo msimu ujao itasaka kurejesha heshima.

POLISI TANZANIA

Ilipanda Ligi Kuu msimu wa mwaka 2020/21 pamoja na Namungo na kumaliza msimu ikiwa nafasi ya sita kwa kuvuna alama 45 huku Simba ikitwaa ubingwa kwa alama 83.

Polisi ilipanda chini ya kocha Mbwana Makata ambaye msimu uliofuata alikwenda kuipandisha Dodoma Jiji na msimu huu ameshuka daraja na Ruvu Shooting.

Maafande hao wamedumu misimu mitatu kwenye Ligi Kuu ambapo msimu huu umekuwa mbovu zaidi kwao kwa kulamiza ligi nafasi ya 15 kwa alama 25 ikishinda michezo sita.

RUVU SHOOTING

Ilishuka daraja msimu wa mwaka 2015/16 pamoja na Polisi Tanzania iliyokuwa inaburuza mkia kwa alama 25 kama ilivyo msimu huu lakini ikarejea tena msimu wa mwaka 2016/17.

Misimu saba kwenye ligi sio michache lakini mambo hayakuwa mazuri msimu huu upande wao kwa kuvuna alam 20 ikishinda michezo mitano na sare tano.

Ilianza msimu chini ya kocha, Charles Mkwasa lakini ikamaliza na Mbwana Makata hivyo msimu ujao mambo yatakuwa mazito kwa timu hizo kila mmoja akisaka kurejea tena Ligi Kuu.

PAMBA FC

Zaidi ya miaka 20 inasota Ligi ya Championship huku ikiwa na matumaini ya kurejea Ligi Kuu baada ya kushuka mwaka 1999 lakini mambo yanawaendea ovyo mwisho.

Utofauti wa alama moja dhidi ya Kitayosce msimu huu ndio umewafanya kusalia tena Championship baada ya kumaliza msimu ikiwa na alama 59 huku Kitayosce alama 60.

Ndio tegemeo la watu wa Mwanza kwa sasa baada ya kupotea kwa Toto African na Gwambina japo ipo Copco kutoka mkoa huo nayo inashiriki Championship huku Alliance ikiwa First League.

MBEYA KWANZA

Inajua utamu wa Ligi Kuu japo iliposhiriki msimu mmoja wa mwaka 2021/22 ikiwa inautumia Uwanja wa Mabatini, Pwani kama uwanja wa nyumbani.

Ilimaliza msimu huo ikiwa inaburuza mkia katika michezo 30 ikishinda mitano na sare 10 na kukusanya alama 25 ambazo zilimshusha daraja pamoja na Biashara United lakini msimu huu imekwama tena.

BIASHARA UNITED

Msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu ilimaliza nafasi ya nne na kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika na kuanza vyema kimataifa.

Ilianza kwa kuichapa 1-0 Dikhil ya Djibouti kisha ikashida nyumbani 2-0 na kukutana na Al Ahli Tripoli ya Libya na kuichapa 2-0 nyumbani lakini ikashindwa kwenda kwenye mchezo wa marudiano.

Biashara ikapokwa pointi na kukumbana na adhabu na msimu uliofuta (2021/22) ikashuka daraja na hadi sasa inazidi kupambana kurudi tena Ligi Kuu ikiwa Ligi ya Championship.

Chanzo: Mwanaspoti