Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita mpya! Simba, Yanga wagongana kwa Diakite

Check Oumar Diakite.jpeg Cheickna Diakite

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga wamezungumza rasmi na winga wa Real Bamako ya Mali, Cheickna Diakite lakini staa huyo ameweka wazi kuwa kuna wakala wa Simba amemcheki wakala wake. Juzi alicheza dakika 45 za kipindi cha pili dhidi ya Yanga, kocha Nasreddine Nabi akateta naye kwa dakika mbili mara baada ya pambano hilo.

Baada ya mchezo huo wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika, Real Bamako ikipoteza kwa mabao 2-0 na mchezaji huyo kufunguka alichozungumza na kocha huyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Diakite amethibitisha kuwa, Yanga inataka huduma yake ambapo hata baada ya kuongea na Nabi ilikuwa ni kumpongeza kwa kiwango chake, pia akimkaribisha kuja kujiunga na klabu hiyo.

Diakite alisema tayari mabosi wa Yanga walimfuata mara baada ya timu hizo kukutana jijini Bamako na pambano baina yao kumalizika kwa sare ya 1-1, ambapo walipeana nafasi ya kuendelea kuzungumza, huku akiitaja Simba pia kumsaka kupitia wakala mmoja wa wachezaji.

“Rasmi naweza kusema Yanga ndio wamenifuata na kuongewa nami, niliongea nao kule nyumbani baada ya mchezo wa kwanza, lakini hata hapa nimeongea na kocha wao (Nabi), ameniambia anapenda kiwango changu nami ni kijana natakiwa kuwa na njaa ya mafanikio kwa kujituma zaidi, amenikaribisha kama nitahitaji changamoto mpya nijiunge nao,” alisema Diakite na kuongeza;

“Ni timu nzuri hapa (Yanga) naona jinsi watu wa hapa walivyo na hamasa, kuna kaka zangu hapa Djigui (Diara) na Mamadou (Doumbia), lakini wakala mmoja pia ameniambia kuna timu inaitwa Simba ya hapa inanihitaji. ”Aidha Diakite amefichua, licha ya kutakiwa na vigogo hao wa Kariakoo klabu yake inapiga hesabu za kumuuza nchini Ufaransa mwisho wa msimu huu ingawa bado dili hilo halijafika mwisho.

“Ilikuwa niondoke muda mrefu lakini waliniambia nisubiri kwanza tumalize msimu huu hasa hizi mechi za CAF, kuna timu ya Ufaransa inazungumza na uongozi wa klabu unajua bado nina mkataba kwahiyo wao pia wataamua ingawa hayo mazungumzo hayakufikia mwisho, nitajua baada ya msimu kumalizika wapi nitakwenda.”

Kocha Nabi anapiga hesabu ya kunasa winga teleza ili kuimarisha kikosi hicho licha ya sasa kuwa na mawinga kama Tuisila Kisinda, Jesus Moloko, Yanga ina mawinga wengine kama Bernard Morrison, Farid Mussa na Dickson Ambundo ambao hawajampa kile anachokitaka. Yanga hesabu zao ni kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano hayo msimu huu na endapo wataifunga Monastir Jijini Dar es Salaam itafuzu robofainali kwa kishindo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live