Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita mbili bado mbichi Serie A

Ac Milan V Torino Fc Serie A Tim Vita mbili bado mbichi Serie A

Sat, 18 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati siku zikizidi kukatika kabla ya Ligi Kuu Italia kumalizika, vita mbili zinaonekana bado mbichi.

Vita hizo ni za kugombania kubaki Ligi Kuu msimu ujao na ile ya kufuzu michuano ya Europa pamoja na Uefa Conference League.

Atalanta iliyopo nafasi ya tano kwa pointi zao 63 ikiwa itashinda mechi zake zote zilizobakia itafikisha pointi 69 ambazo zitawahakikishia kufuzu Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi.

Lakini kama Atalanta itaangusha alama inaweza kutupwa nafasi ya sita na kujikuta ikishiriki Europa League badala ya Ligi ya Mabingwa kwani wapinzani wao AS Roma wapo karibu yao.

Fiorentina ambayo ipo nafasi ya nane na pointi zao 53 inapambana vilivyo na Napoli katika vita ya kufuzu Uefa Conference Legaue na kama ikiangusha alama na Napoli iliyopo nafasi ya tisa ikashinda mechi zake zote zilizobakia inaweza ikawaondoa kufuzu michuano hiyo.

Lakini Fiorentina sio tu inapambana kufuzu Uefa Conference League bali inaweza kushiriki Europa League msimu ujao ikiwa itashinda mechi zake zote zilizosalia na kufikisha pointi 62, zinazoweza kuzivuka timu moja kati ya Lazio na Roma ikiwa hazitofanya vizuri katika mechi mbili za mwisho.

Kwa upande wa vita ya pili ya kuwania kubaki, Sassulo yenye alama 29 katika nafasi ya 19 na Udinesse yenye alama 30 katika nafasi ya 18, zote zina uwezo wa kujiondoa katika eneo hilo ikiwa tu, timu zilizo juu yao zitangusha walau pointi mbili au tatu.

Sassuolo ambayo imeshacheza mechi 36, ikibakisha mechi mbili, ikishinda hizo inaweza kupanda hadi nafasi ya 14 ikiwa Verona iliyopo nafasi hiyo itafungwa katika mechi zao mbili za mwisho.

Au kama sio Verona, Sassuolo inaweza kuzishusha Cagliari, Frosinone na Empoli ikiwa hizi nazo zitafanya vibaya katika mechi hizi zilizobakia.

Hali ipo hivyo pia kwa Udinese ambayo kama itashinda mechi mbili zilizobaki inaweza kupanda na kufika hadi nafasi ya 14 ikiwa Verona itafanya vibaya.

Kwa sasa Udinese ina alama 30.

Chanzo: Mwanaspoti