Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita kupanda Ligi Kuu yazidi kunoga kwa Pamba, Geita Gold

Pamba Pic Data Vita kupanda Ligi Kuu yazidi kunoga kwa Pamba, Geita Gold

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mwanza. Huko kundi B kwenye Ligi Daraja la Kwanza moto unaendelea kuwaka kwa miamba ya soka kanda ya ziwa kwenye vita ya kupanda Ligi Kuu kufuatia ushindi mnono walioupata leo katika mechi zao.

Timu hizo Pamba (Mwanza) na Geita Gold ya mkoani Geita zinafukuzana vikali katika harakati za kuungana na Simba na Yanga msimu ujao.

Katika mechi za leo Jumapili, Pamba ikiwa dimba la Nyamagana kukipiga dhidi ya majirani zao, Alliance wameiburuza mabao 3-0 na kuendelea kukaa kileleni kwa pointi 28, huku wapinzani wao wakibaki mkiani kwa pointi tano.

Pamba wakicheza kwa kasi dakika 45 za kwanza, waliweza kuandika mabao kupitia kwa Reward Macha dakika ya 28 na Emanuel Haule kuweka la pili dakika 39 na kwenda mapumziko wakiongoza kwa idadi hiyo.

Kipindi cha pili Alliance ilijaribu kujitutumua kutaka kusawazisha mabao hayo lakini dakika ya 79 wakajikuta wakipachikwa la tatu kupitia kwa Moses Msukanywele na kuwazamisha zaidi wapinzani hao.

Wakati Pamba ikifanya 'mauaji' hayo, nao Geita Gold wameinyuka vikali Mbao FC kwa kuwanyoa mabao 3-0 na kubaki nafasi yao ya pili kwa alama 26.

Related Magera Cup kuliamsha Rock City, timu nane kukinukishaKatika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Nyankumbu mjini humo, mabao ya Lambere Jerome aliyetupia mawili na Venace Ludovic yalitosha kabisa kuizima Mbao ambao wanahatihati ya kushuka daraja kutokana na kuwa nafasi mbili za mwisho kwa alama saba.

Hata hivyo baada ya mechi ya Pamba na Alliance kumalizika ilishuhudiwa viongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA) wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Vedastus Luphano sambamba na Meya wa Jiji, Costantine Siima wakitoa hamasa na pongezi kwa vijana wa TP Lindanda.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz