Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita Yanga vs Azam haijaisha bado!

Azam Tanga Vita Yanga vs Azam haijaisha bado!

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama umepanga kuikosa mechi ya Ngao ya jamii kati ya Mabingwa wa nchi Yanga dhidi ya Azam utafanya makosa makubwa kwani bato hilo limeanza leo Agosti 8 kabla ya siku ya mchezo.

Picha limeanzia kwenye tukio la klabu zote kuja kuukanyaga Uwanja wa mchezo pale CCM Mkwakwani na wa kwanza kufika hapo walikuwa Yanga wakitinga majira ya saa 10:28 jioni.

Yanga kama kawaida kikosi chao Cha ulinzi maarufu kwa jina la Task Force kilishakuwa tayari kuanzia nje kuipokea timu yao kisha basi lao likaingia moja kwa moja mpaka ndani na wachezaji wao kushuka na kuingia uwanjani.

Dakika mbili baadaye matajiri wa Chamazi nao wakatinga uwanjani hapo wakiwa ndani ya basi lao la bei mbaya Irizar na safari hii likaingia kwa mbele ndani ya geti hilo.

Baada ya basi la Azam kuingia mzozo ukaibuka kati ya walinzi wa Yanga na wale wa Azam ambapo Azam walitaka kwenda kupaki ubavuni mwa basi la wapinzani wao.

Walinzi wa Azam wakataka pia wachezaji wao wapite geti hilo la kwanza hatua ambayo wenzao wa Yanga wakaigomea na kuanza kusukumana lakini hata hivyo Yanga wakashinda vita hiyo.

Azam wakabadili akili na kuamua kufunika kombe na kwenda kupita mlango mkuu wa kuingilia jukwaa kuu kisha wakaingiza ndani ya uwanja.

Wakati wachezaji wa Azam wakiingia uwanjani hapo wakapishana na wenzao wa Yanga wakiwa wanatoka.

Yanga leo Agosti 9 itakutana na Azam katika mchezo wa kwanza wa kuwania ngao ya jamii, mechi ikipangwa kuanza saa 1:00 usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live