Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Visit Rwanda" yaingiza zaidi ya Trilioni 1

Visit Rwanda "Visit Rwanda" yaingiza zaidi ya Trilioni 1

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rwanda imeingiza kiasi cha ($445 million) zaidi ya TSh. Trilioni 1 kupitia sekta ya utalii kwa mwaka 2022 ambapo inaripotiwa jumla ya watalii milioni 1 walitembelea taifa hilo la Afrika Mashariki.

Haya ni matunda ya ushiriki wao kwenye Kampeni ya “Visit Rwanda” ambayo wameingia makubaliano na Klabu ya Arsenal pamoja na PSG. Mwaka jana Rwanda waliingia mkataba wa (£10 million) zaidi ya TSh. Bilioni 28 kwa mwaka na Arsenal kwa ajili ya kuweka bango hilo kwenye jezi zao kwa miaka Minne.

Kwa PSG ya Ufaransa vile vile, inaripotiwa kuwa mwaka 2019 walisaini dili la miaka mitatu lenye thamani kati ya (€8 -10 million) zaidi ya TSh. Bilioni 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live