Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ilimbidi kusubiri kwa siku tano ili kupata visa ya kurejea Saudi Arabia kwa ajili ya kwenda kutekeleza majukumu yake ya kuichezea klabu ya Al-Qadsiah inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo.
Awali, Msuva ilibidi kuondoka nchini Alhamisi ya Machi 30, lakini ikashindikana hivyo ikabidi safari yake kusogezwa mbele hadi leo Alhamisi Aprili 6, 2023.
Msuva alisema hiyo ilikuwa sababu iliyo nje ya uwezo wake hivyo waajiri wake ilibidi waelewe licha ya kwamba walitaka kumwona akirejea mapema ili kuuwahi mchezo wa ligi dhidi ya Al-Ain ambao ulichezwa jana huku love wakiambulia kichapo.
Chama la Msuva ni kati ya timu nne ambazo zipo kwenye nafasi za chini kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia, na kwenye hatari ya kushuka daraja.