Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Virgil Van Dijk: Ushindi dhidi ya Newcastle umeturudisha relini

Van Dijk VVD Virgil Van Dijk: Ushindi dhidi ya Newcastle umeturudisha relini

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa klabu ya Liverpool Virgil Van Dijk ameutafsiri ushindi walioupata dhidi ya klabu ya Newcastle katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza inaweza kua njia ya wao kurudi kwenye ubora wao.

Klabu ya Liverpool jana imefanikiwa kupata ushindi 2-0 dhidi ya klabu ya Newcastle United na kutimiza ushindi wa pili mfululizo baada ya kuifunga klabu ya Everton siku ya jumatatu katika derby ya Merseyside, Ushindi huo umeleta taswira ya tofauti kwa beki wa klabu hiyo Virgil Van Dijk.

Klabu ya Liverpool imekua kwenye wakati mgumu msimu huu wakiwa nafasi ya nane katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama zao 35, Huku wamefanikiwa kushinda michezo 10 kati ya michezo 22 ambayo wamecheza mpaka sasa msimu huu.

Beki Virgil Van Dijk anasema wameshinda michezo kadhaa msimu huu lakini ushindi dhidi ya Newcastle United umempa hisia ya tofauti, Kwani anaamini kwanza wamecheza na timu bora sana ambayo inafanya vizuri msimu huu pia wanakua timu ya pili kuifunga Newcastle msimu huu.

Van Dijk pia ameusifu ushindi wa Liverpool kwani wamecheza na moja ya timu ngumu zaidi msimu huu kwenye ligi kuu ya Uingereza, Hivo kupata ushindi dhidi ya klabu ya Newcastle limekua jambo kubwa kwao na anaona kama mwanzo wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo kuelekea michezo mingine ya klabu hiyo inayofata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live