Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vipigo vyamkimbiza Masau Bwire kuzishabikia Simba, Yanga

Masau Bwireee Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire

Tue, 12 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waswahili wanasema ukishangaa ya Musa, utastaajabu ya firauni. Ndivyo ilivyotokea kwa Afisa Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire.

Wakati wa ukuaji wake Masau alipitia ushabiki wa kuvishabikia vilabu vikongwe hapa nchini Simba na Yanga, kama ilivyo utamaduni wa wengi.

Ipo hivi, Masau alianza kuishabikia Simba SC kutokana na kumuona kaka yake aliyekuwa akiitwa Isaya Bwire ambae alikuwa shabiki wa Mnyama kindaki ndaki.

Huyu ndie aliemrithisha Masau Kuipenda Simba, lakini ndie aliemfanya kuichukia Simba baada ya kuharibu picha za wachezaji wa Simba alizokuwa amezibandika katika chumba chake.

"Huyu kaka yangu alibandika picha za wachezaji wa Simba chumbani kwake, sasa mimi kutokana na utoto nikaenda kuzitoboa macho alipogundua ni mimi alinikimbiza kijiji kizima na kunipiga sana hivyo nikashika chuki na kuichukia Simba kwa kile kilichonikuta"

Mkasa huo ulimfanya Masau kuhamia Yanga akimfuata Kaka yake mwingine kutokana na kwamba kwao walizaliwa watoto 20, hivyo hata katika ngazi ya familia walikuwa wamegawanyika, kuna waliokuwa wanaishabikia Simba na wengine Yanga.

Masau akaamua kumfuata Kaka yeke mwingine aliekuwa anaitwa Elisha Kuliga ambae alikuwa Shabiki lia lia wa Yanga.

Kilichomkimbiza kwa Wananchi nacho ni kipigo vile vile baada ya siku moja kupanga kucheza mchezo wa Simba na Yanga katika timu zao za mtaani, hivyo akabaki kucheza mpira na kutega kwenda shule ili akacheze mechi ya mtani.

"Siku ya pili nilivyokwenda shule namkumbuka Mwalimu wangu wa hesabu sasa hivi ni marehemu, akaita wale wote ambao hawakufika shuleni siku iliyopita, aisee yule bwana alinipiga sana na kila nikifikiria kipigo chote hiki ni kwa ajili ya Yanga, nikashika chuki na kuhama Yanga moja kwa moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live