Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vipigo inavyotoa TP Mazembe kwa vigogo hapo Lubumbashi mhh! Simba ijipange kweli

51591 Pic+simba+mazembe

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Simba ina kibarua kigumu ugenini dhidi ya TP Mazembe, Jumamosi saa 9.00 Alasiri wakitakiwa kushindi au sare ya mabao ili iweze kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita timu hizo zilitoka suluhu hivyo mshindi wa jumla wa mechi mbili baina ya timu hizo atakutana na mshindi baina ya Esperance na CS Constantine.

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa TP Mazembe uliopo jijini Lubumbashi na utachezeshwa na mwamuzi Janny Sikazwe kutoka Zambia.

Hata hivyo Simba wana mtihani mgumu kupata matokeo ugenini mbele ya TP Mazembe kwani wapinzani wao wamekuwa na rekodi nzuri ya kuibuka na ushindi pindi wanapokuwa uwanja wa nyumbani.

Simba wanapaswa kujipanga vilivyo kwani Mazembe wamekuwa na rekodi ya kutoa vipigo kwa timu mbalimbali iwe kubwa au ndo na kwa kulithibitisha hilo, makala hii inakuletea vipigo vitano ambavyo vigogo mbalimbali vya soka Afrika vilikutana navyo pindi zilipocheza na TP Mazembe ugenini.

TP Mazembe 8-0 Club African (2019)

Ikiwa imetoka kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Ismaily ya Misri, timu ya Club Africain kutoka Tunisia ilijikuta ikipokea kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa TP Mazembe kwenye mechi ya mzunguko wa tatu wa kundi C la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu iliyochezwa huko Lubumbashi.

Beki Kevin Mondeko na washambuliaji Tresor Mputu na Jackson Muleka kila mmoja alifunga mabao mawili kwenye mchezo huo wakati Michee Mika na Meschak Elia walifumania nyavu mara moja.

TP Mazembe 4-1 ES Setif

Mabingwa wa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1988 na 2014, ES Setif ya Algeria, mwaka 2018 walikutana na dhahama ya kucheza na Mazembe ugenini baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Stade TP Mazembe.

Mabao ya Ben Malango aliyefunga mawili, Elia Meschak na Nathan Sinkala yalitosha kuwazamisha Setif kwenye mchezo huo uliokuwa wa kundi B.

TP Mazembe 5-0 Al-Hilal Al-Ubayyid

Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Al-Hilal Al-Ubayyid ya Sudan, TP Mazembe ilijihakikishia kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2017 kwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 kwenye mechi ya marudiano nyumbani.

Wafungaji wa mabao hayo matano ya Mazembe siku hiyo walikuwa ni Jean Kasusura, Ben Malango, Elia Meschak, Issama Mpeko na Adama Traore.

TP Mazembe 5-0 Moghreb Tétouan

Wawakilishi wa Morocco, Moghreb Tetouan mwaka 2014 nao walikutana na kisago cha haja pindi walipotua Lubumbashi kucheza na TP Mazembe ambapo walichapwa mabao 5-0.

Nyota wa zamani wa Mazembe anayechezea Genk ya Ubelgiji alipachika mabao matatu kwenye mchezo huo huku mengine mawili yakifungwa na Rainford Kalaba na Roger Assale.

TP Mazembe 3-0 El Merrikh

Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 nyumbani kwenye mechi ya hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2015, El Merrikh ilitandikwa mabao 3-0 kwenye mechi ya marudiano na kutupwa nje ya mashindano hayo.

Walikuwa ni Mbwana Samatta na Roger Assale waliofumania nyavu huku lingine likiwa la kujifunga la mchezaji wa El Merrikh, Moseeb Omer.

TP Mazembe Vs Simba



Chanzo: mwananchi.co.tz