Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wakubali kuwajibika ili Azam FC isonge mbele

Zakazakazi Hj.jpeg Mkuu wa Kitengo cha Habari Azam FC, Thabit Zakaria

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nimepitia kurasa mbalimbali za mitandao ya Kijamii, nimepitia ukurasa wa Azam Fc na Viongozi wao na sijaona ishara ya uwajibikaji. Kama kweli wanaipenda hii timu basi watoke na washabikie sababu kuiongoza wameshindwa.

Nafikiri sio lazima wafukuzwe, nafikiri bodi ingekaa na kujiona wamefeli PROJECT yao na wenyewe wakabwaga manyanga watu wengine wachukue hatamu. Hakuna namna inaelezeka kwa nini sio washindani Afrika..?

Kama watabaki viongozi hawa waliopo sioni namna Azam Fc itafurukuta msimu huu, nawaona wakiendelea kuwa wapiga ZUMARI kusindikiza wenzao. Watabaki kutazama michuano ya Kimataifa kwenye Uwanja wao.

Kama PROJECT Manager ambaye ni CEO amekwama maana timu yake yote chini imekwama hivyo anapaswa kufungasha vilago na kukabidhi ofisi. Wao ndio wanapaswa kuisaidia hii timu kwa kuiacha kuliko kung’ang’ana.

Unakuwaje na timu kama Azam Fc yenye kila kitu halafu hakuna namna mnafanikiwa..? Yaani Azam Fc inapaswa kuwa kama TP Mzembe ile au Pyramids Fc. Azam Fc inapaswa kuwa kielelezo cha Uwekezaji kwenye Soka letu.

Kuwajibika kwa kuachia nafasi na yenyewe ni sehemu ya Utatuzi wa Tatizo..? Kwa Timu yenye uwezo wa kila kitu inashindwaje kufanikiwa haswa KIMATAIFA..? Labda hapa watasema Usimba na Uyanga.

Timu ina miundombinu, ina uwezo wa kulipa wataalam, uwezo wa kusajili wachezaji na kila aina ya uwezo wa kiuendeshaji kisha siku Ya Tatu baada ya Aibu hakuna aliyeng’oka wala ishara ya Kujali.

Waachie Nafasi, Watu wengine waanze mchakato. Hata wapewe miaka 100 kama Mindset zao ndio hizi basi hakuna namna watafanikiwa, waondoke. Nimewaza namna wenzao huwa wanapagawa wakishindwa.

Ameandika Biko Armando Scanda

Chanzo: www.tanzaniaweb.live