Nimependa namna ambavyo viongozi wa Yanga kuanzia wale wa juu hadi hawa watendaji wao wa chini kuna kitu kimebadilika kwa namna wanavyozungunza pindi wanapowekewa vipaza sauti.
Tangu Ofisa Habari wao Ally Shaabani Kamwe amkosee heshima Kocha Juma Mgunda kwa sasa viongozi wa juu hadi wa chini wamekuwa na staha (Kauli nzuri) katika kuzungumza.
Kumbuka wakati ule Henock Inonga alivyomchezea rafu mbaya Abubakar Salum Sure Boy hukusikia wakisema ile ilikuwa makusudi. Ni majuzi tu Joyce Lomalisa alichezewa rafu mbaya na Hashim Manyanya wa Namungo FC wala hukusikia viongozi wa Yanga wakisema ile ilikuwa makusudi.
Kuna namna nawaona viongozi wa Yanga hawajiingizi katika Lugha za kishabiki hasa baadhi ya mambo yanapotokea katika klabu yao.