Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Simba wana deni hapa

Zrane Dead (1).jpeg Viongozi wa Simba wana deni hapa

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye zoezi la kuuaga mwili wa Adel Zrane pale Rwanda watu mbali mbali walitoa speache zake akiwemo Amine Zrane kaka yake ambaye huyu alilia muda wote wa speeach yake, akafuatia mke wake @mahoutamaya aliongea maneno mazito ambayo yaliwaliza watu wengine

"Akisema Mume wangu wewe ni mtu wa pekee sana ambaye nilikuwa nikimuomba Mungu anipe wakati wote , umeondoka lakini tambua nitakupenda na nitakuwa na wewe milele , umewaacha watoto ambao milele watajivunia kuwa na Baba bora , Nakupenda sana Adel '' ni maneno ambayo yaliwaliza wengine sana

Hapa viongozi wa Simba kama itawapendeza Kiongozi mmoja awe Ahamedy Ally , awe Shabiki wa Simba aende Tunisia kuwapa faraja maana hata ndugu zake wengi walikuwa wanajua yupo Tanzania hawakuwa wanaijua sana Rwanda

Litakuwa Jambo la busara sana kwa kuwa ni kipenzi cha mashabiki wa Simba wanampenda na watampenda ni vyema kungelitumwa muwakilishi aende kwenye mazishi yake hapo Tunisia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live