Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Simba ni wazembe

Murtaza Mangungu Viongozi wa Simba.

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa kawaida mchezaji mzuri siku zote huwa anapokaribia kumaliza mkataba wake basi klabu kama Bado inahitaji huduma yake huwa unaanza kufanya mazungumzo ya kumuongezea mkataba mwingine mpya mapema ili kutokuwa na hizi changamoto ambazo Kwa Sasa klabu ya Simba inapitia Kwa Kibu Denis.

Mfano, klabu ya Chelsea FC ina mchezaji anaitwa Conor Gallagher katika mkataba wake amebakiza mwaka mmoja na nusu ambapo mkataba wake unafikia mwisho mwaka 2025 mwezi wa sita, lakini tayari klabu yake Kwa sababu Bado inahitaji huduma yake mchezaji basi wameshaanza mazungumzo ya kuboresha zaidi mkataba wake ili aendelee kusalia ndani ya klabu.

Klabu ya Simba kupitia Kwa viongozi wake Kuna namna fulani wamekuwa wazembe katika kumalizana na hili dili mapema, mchezaji ni wao tena halali lakini Kwa hali inavyozidi kusonga basi watajikuta wanamkosa hivi hivi kama masihara.

Huwezi ukawa na mchezaji kama Kibu Denis halafu hadi Sasa hivi akiwa amebakiza mwezi mmoja mkataba wake uishe halafu ukawa hujamuongezea mkataba.

Ndiyo najua Kuna mambo mchezaji atataka kuboreshewa lakini Bado Kwa klabu yenye viongozi makini masilahi ya mchezaji kuyaboresha lazima uboreshe na hili ni jambo la kawaida Sana Kwa kila timu na Kwa Kila mchezaji.

Dirisha liko mbioni kufunguliwa, presha inazidi kuwa kubwa Kwa sababu wote tunajua siasa za soka la bongo zinavyokuwa. Na Kwa bahati mbaya zaidi wakala wa Kibu Denis ndiyo huyu huyu pia ana wachezaji upande wa pili akiwa anawasimamia.

Kwa hiyo huwezi kushangaa kama akiwaambia Simba SC kuwa mteja wake amepokea ofa kubwa kutoka Yanga SC na hili ni jambo la kawaida kabisa wakati huu kuelekea kufunguliwa Kwa dirisha la usajili, kwa hiyo viongozi wanatakiwa kuwa makini ili kuepuka kumgombanisha Kibu Denis na mashabiki wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live