Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Simba nao wanasikitika

Simba Mtihani Mzito Dhidi Ya Jwaneng Galaxy Wikiendi Hii.jpeg Viongozi wa Simba nao wanasikitika

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa matokeo ambayo wameyapata kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas sio mazuri kwa upande wao kwa namna yoyote.

Novemba 25 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi.

Kwenye msako wa pointi tatu Simba ilikomba moja ikiwa nyumbani na kupoteza pointi mbili muhimu.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema sio matokeo mazuri kwao kwa kuwa hayakuwa malengo yao kwa namna hiyo.

“Tulikuwa nyumbani tuliamini kwamba ni muhimu kupata pointi tatu. Kwetu kupata pointi moja tumepoteza hivyo hatujapenda tutafanyia kazi makosa yaliyotokea.

“Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hesabu kubwa ni kupata pointi kwenye mechi za nyumbani. Kwa namna ambavyo tumeanza tuna wakati wa kujipanga ili kupata ushindi kwa mechi zijazo,”.

Mchezo ujao wa Simba kimataifa ni dhidi ya Jwaneng Galaxy unatarajiwa kuchezwa Botswana, Desemba 2 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live