Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi Yanga waenda kulilia Goli lao CAF

Gsm 0 Viongozi Yanga waenda kulilia Goli lao CAF

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kukataliwa kwa goli la kiungo wake Stephen Aziz KI katika mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Mamelodi mchezo ambao umewashuhudia Yanga wakiaga Mashindano hayo.

Uongozi wa Yanga umepanga kuandika barua ya kueleza malalamiko yao kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF.

Hilo limethibitishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma ambae kupitia ukurasa wake wa X ameandika;

Nimetoka kuongea na viongozi wa @YoungAfricansSC na tumekubaliana wanaiandikia CAF kulalamika kuhusiana na goli la wazi lililokataliwa. Haitabatilisha matokeo,lakini angalau tuweke kumbukumbu sawa na ikithibitika hata mwamuzi achukuliwe hatua stahiki. LILE LILIKUWA GOLI HALALI.

Je Unadhani Yanga watafaidika na lolote kwa maamuzi hayo, Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: