Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi Simba kukutana na mashabiki kujadili mwenendo wao

Simba Ndio Sababu Ya Marekebisho Ya Uwanja Wa Mkapa   Try Again.jpeg Viongozi Simba kukutana na mashabiki kujadili mwenendo wao

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba SC, umesema utakutana na baadhi ya wanachama wao kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu klabu yao.

Akizungumza na Azam TV, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salum Abdallah Try Again, amesema anawashukuru mashabiki na wanachama wa Simba kwa kuendelea kuiamini klabu licha ya kutoka kupoteza mchezo dhidi ya Yanga SC lakini pia kumpoteza Kocha Mkuu Roberto Oliviera 'Robertinho'.

Alisema kwa sasa mashabiki wa Simba kwa sasa wanatakiwa kushikamana, kujiandaa na mchezo wa ASEC Mimosas utakaochezwa Novemba 25, 2023 mchezo wa hatua ya Klabu Bingwa Afrika.

"Nilipokea email ya mashabiki wakiomba kukutana na uongozi wangu, hii kwetu ni jambo zuri sana. Nimeona barua ile imesainiwa na Ustaz Masoud, Don King, Haruna Nazi na watu kama saba nane hivi. Tumepokea maoni yao waliyoyaandika tutayafanyia kazi lakini pia kukutana nao," alisema Try Again.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live