Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viola wamsubiri Amrabat wao

Ten Hag With Amrabat Viola wamsubiri Amrabat wao

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Fiorentina inajiandaa kumpokea kiungo wao Sofyan Amrabat atakayerejea kikosini mwishoni mwa msimu huu baada ya mambo yake kwenda hovyo huko Manchester United, imeelezwa.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco, Amrabat, 27, alijiunga na Man United kwa mkopo a msimu mmoja utakaofika tamati wakati wa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Amrabat alitarajiwa atafanya mambo kwenye kiungo ya Man United hasa ukizingatia aliwahi kuwa chini ya kocha Erik ten Hag walipokuwa pamoja Utrecht kati ya mwaka 2015 na 2017.

Lakini, mashabiki wa Man United wameshindwa kupata huduma bora ya staa huyo, ambapo Ten Hag wakati mwingine amekuwa akimbadilishia nafasi na kucheza kwenye beki ya kushoto.

Amrabat amejikuta akipoteza nafasi mbele ya kinda Kobbie Mainoo, ambaye kwa sasa panga pangua amekuwa chaguo la kwanza la kocha Ten Hag kwenye kikosi hicho chenye maskani yake Old Trafford.

Man United ilitoa Pauni 8 milioni kulipia mkopo wa Amrabat. Katika dili hilo, Man United inaweza kumchukua jumla kiungo huyo kwa ada ya Pauni 17 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 4.2 milioni.

Lakini, Desemba mwaka jana ilifichua kwamba Man United haina mpango wa kumchukua Amrabat jumla baada ya kuibuka kwa Mainoo, habari ambazo zimepokewa kwa shangwe huko Italia, ambapo Fiorentina wanamsubiri arudi baada ya kuanzishwa kwenye mechi saba tu kati ya 27 zilizochezwa kwenye Ligi Kuu England msimu huu, huku mechi sita alitokea kwenye benchi.

Chanzo: Mwanaspoti