Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vinicius Jr apewa uraia wa Hispania

Vinicius Jr  . Vinicius Jr

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Real Madrid ya Hispania imethibitisha kuwa winga wao Mbrazil, Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior maarufu kama Vinicius Jr au Vini Jr (22) rasmi amepewa uraia wa Hispania, Klabu yake imethibitisha.

Vinicius amepewa uraia huo, Septemba 2, 2022 baada ya kuapa mahakamani kutokana na Real Madrid kubanwa na sheria ya La Liga inayoruhusu kutumia wachezaji watatu tu wanaotoka nje ya nchi za Umoja wa Ulaya ndani ya mechi moja.

Uwepo wa Vinicius Jr, Militao, na Rodrygo ulikuwa unafanya mlinzi wa kulia Vinicius Tobias (18) ashindwe kuitumikia timu hiyo. Aidha, klabu hiyo inataka kusajili mchezaji mwingine nje ya Ulaya kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Mpaka sasa ni wachezaji wawili Federico Valverde (Uruguay & Hispania) pamoja na Vinicius Jr (Brazil & Hispania), ndio wachezaji wa Real Madrid waliopewa uraia wa Hispania.

Katika hatua nyingine klabu hiyo pia imeanza mchakato wa kuhakikisha Militão na Rodrygo wanapata uraia wa nchi hiyo pindi watakapofikisha kipindi cha miaka mitano cha kucheza Ligi hiyo ili kukamilisha vigezo vya kupata uraia.

“Real Madrid CF inawatangazia kuwa, sasa ni rasmi mchezaji wetu raia wa Brazil, Vinicius Junior ameapa kwa mujibu wa katiba ya Hispania, Ijumaa, Septemba 2, kuanzia sasa atakuwa pia raia wa Hispania,” imesema taarifa hiyo.

Vinicius ambaye mwaka 2018 alijiunga na mabingwa hao wa UEFA akitokea Flamengo, mpaka sasa amecheza mechi 176 akifunga mabao 40 na pasi za mwisho 45, hivyo sasa atasomeka kama mchezaji wa ndani wa Hispania lakini hatoruhusiwa kuchezea timu ya taifa ya Hispania kwa sababu tayari ameshachezea timu ya taifa ya Brazil.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live