Mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil, Vinicius Jr ametoa kauli hii rasmi ya kumuunga mkono Benjamin Mendy.
"Samahani kwa yote uliyopitia Benjamin mendy. Ulipoteza miaka miwili ya kazi yako.
Vipi kuhusu uharibifu wa kisaikolojia? Hakika maisha yako hayatakuwa sawa kamwe. Utamaduni wa kuharibu sifa utakufanya kua mwathirika mwingine.
Mpaka lini tutashtakiwa na kisha tukahukumiwa bila kuwa na haki ya ulinzi wa msingi?
Habari za uongo hutengenezwa na kuenea bila kuangalia ukweli wowote (ambao ni jambo binafsi nilitafakari sana kwenye likizo hii) halafu hali inakuwa mbaya zaidi upande wetu sisi mastaa.
Kuwajibika itakuwa chini kwa mtu yeyote, lakini siku hizi kazi kubwa imekuwa ubaguzi. Swali langu ni je, nini itafanywa kurekebisha uharibifu huu unaoendelea?
Vinicius asema haya yote baada ya Paul Pogba na Memphis Depay ambao tayari walimuunga mkono Benjamin Mendy baada ya kukutwa hana hatia na kesi yake iliyokua ikimkabili.
Ikumbukwe kwamba Mendy alikutwa hana hatia ya katika mashtaka mawili yaliyokuwa yakimkabili moja la ubakaji na lingine la kujaribu kubaka.
Mendy (28) alibubujikwa na machozi maamuzi hayo yalipotolewa na msimamizi wa Mahakama ya Chester Crown Kaskazini Magharibi mwa Uingereza Julai 2023.