Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vinicius Jr: Nilimshawishi Bellingham kuja Madrid

Vini Jr 116.png Vinicius Jr: Nilimshawishi Bellingham kuja Madrid

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Jr alimtumia meseji Jude Bellingham kila siku kwa muda wa mwaka mzima ili kumshawishi ajiunge na timu hiyo.

Nyota huyo wa kimataifa wa England alitua La Liga kutoka Borussia Dortmund kwa Pauni 115 milioni na tayari amekuwa na mchango mkubwa.

Madrid ilizishinda timu za Ligi Kuu England katika kinyang’anyiro cha kuwania saini yake zikiwemo Liverpool, Manchester City na Manchester United kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20.

Bellingham amefunga mabao manane katika mechi tisa alizocheza Los Blancos huku akitoa asisti tatu na kuwa kivutio zaidi katika kikosi cha Carlo Ancelotti msimu huu.

Sasa winga wa Madrid, Vini ametoboa siri baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi SSC Napoli katika mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya juma hili kwamba aliwasliana na Bellingham kila siku akimuomba akubali kutua Santiago Bernabeu.

“Nilimuhitaji Bellingham hapa (Madrid). Nilimtumia meseji kla siku mwaka jana. Ilikuwa haipiti siku bila ya kumtumia meseji, nilikuwa namwambia njoo Madrid.” alibainisha Vini.

Naye Bellingham alimsifia mchezaji mwenzake Vinicius akidai anajivunia kucheza pamoja naye: “Nadhani ni mchezaji bora duniani kwa upande wangu. Ni miongoni mwa wachezaji wenye vipaji ambao nimewahi kucheza nao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live