Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vinicius, Barcelona waingia katika vita ya maneno

Wanne Wakamatwa Kwa Kutundikwa Kwa Sanamu Ya Vinicius Jr Vinicius Jr

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya Barcelona amekanusha kwa mshangao kwamba Vinicius Jr amekuwa akikabiliwa vitendo vya kibaguzi.

Pia, amedai nyota huyo wa Real Madrid “anastahili kupigwa kofi,” kutokana na aina ya uchezaji wake uwanjani.

Mfanyakazi huyo wa Barcelona anayeitwa Mikel Camps alizungumza kauli hiyo dhidi ya Vinicius Jr kupitia akaunti yake ya X baadaye akafuta alichokiandika. Aliandika:

“Sio vitendo vya kibaguzi anastahili kupigwa makofi kwa ujinga wake. Anajaribu kuwakilisha nini uwanjani?

Kufuatia kauli hiyo Mkurugenzi wa Barcelona, Rafa Yuste amekiri kwamba kauli hiyo haikupaswa kuandikwa kwa namna hiyo.

“Kama Vinicius atanisikiliza mimi, nitamwambia jambo kama halitajirudia tena. Hata kama ulimi umeteleza jambo kama hilo halitatokea tena.” Vinicius Jr mara kwa mara amekuwa akikabiliwa na ishu za ubaguzi wa rangi kutoka kwa mashabiki wa wapinzani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live