Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vini Jr, Mbappe nani mfalme mpya Real Madrid?

Vinicius Mbappe Vini Jr, Mbappe nani mfalme Real Madrid

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Real Madrid kutangaza kumsajili Kylian Mbappe kwa mkataba wa miaka 5, akitokea PSG akiwa mchezaji huru. Maswali yanayokuja sasa ni namna gani Mbappe ataingia kwenye kikosi hicho na muonekano wa Real Madrid kiwanjani utakuwaje.

Moja ya swali kubwa ni namna gani Vinícius Júnior na Mbappe watacheza kwenye kikosi hicho kwenye nafasi za uchezaji, wachezaji wote wawili ni bora zaidi wakicheza kutokea upande wa kushuto. Ingawa Mbappe anauwezo pia wakucheza kama mshambuliaji wa kati japo mikimbio yake mingi huwa kutokea upande wa kushoto.

Jambo jingine Vinícius Júnior ni moja ya wachezaji wenye ushawishi mkubwa ndani ya real Madrid kwenye eneo la ushambuliaji na ndio mfungaji bora wa Madrid msimu 2023-24 akiwa na bao 24 kwenye michuano yote. Ujio wa Mbappe unatengeneza swali jingine nani atakuwa Mfalme wa Real Madrid kati ya wachezaji hawa wawili?

Kibarua kinabaki kwa kocha Carlo Ancelotti namna gani atapanga kikosi chake.

Chanzo: Mwanaspoti