Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Villareal yatinga Nusu Fainali UEFA kibabe

Villareal Winner Villareal yatinga Nusu Fainali UEFA kibabe

Wed, 13 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao la Mshambuliaji wa Kimataifa wa Nigeria Samuel Chukwueze limeipeleka Villarreal hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Bayern Munich matokeo ya jumla ingawa mchezo wa mkondo wa pili uliochezwa jana Jumanne dimba la Allianz Arena umemalizika kwa sare ya goli 1-1.

Licha ya Nyambizi hao wa Njano Villarreal kwenye mechi zote mbili wamepiga mashuti mawili tu golini dhidi ya Bayern Munich katika hayo mashuti yote mawili yamezaa magoli. Shuti la kwanza lilizaa goli Hispania kisha shuti la jana usiku limezaa bao la kusawazisha.

Baada ya kiwango kizuri nyumbani na kuondoka na ushindi wa bao 1-0, vijana wa Unai Emery wameonyesha nidhamu kubwa katika ulinzi raundi ya pili mpaka dakika za mwishoni 88 ambapo kijana wa Kinigeria Chukwueze alipofunga bao la sare lakini lenye kufikia ushindi ambao unaipeleka nusu fainali ya kwanza baada ya miaka 16.

Bao la Bayern Munich kwenye mechi ya jana limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski dakika za kipindi cha pili likiwa ni bao lake la 13 kwenye mashindano hayo pia inakuwa timu ya 30 kuifunga goli kwenye mashindano ya UEFA ambapo sasa ni wachezaji wanne pekee (Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Karim Benzema na Raul )ambao wamezifunga timu zaidi ya 30.

Baada ya ushindi huo, Villarreal watacheza na mshindi mmoja wapo kati ya Liverpool na Benfica ambao watacheza leo Jumatano Aprili 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live