Katika Mashindano ya CAF kwa Vilabu msimu huu 2023-2024 jumla nchi wanachama 45 zimethibitishwa na CAF kushiriki na kuweza kutoa jumla ya Timu 106 zilizothibitishwa na CAF kati ya hizo Timu 54 katika CAF Champions League na Timu 52 katika CAF Confederation Cup.
Kati ya nchi 45 zinazoshiriki nchi 42 Timu zao zinashiriki Champions league bila uwepo wa nchi 3 nazo ni Kenya, Madagascar na Seychelles wakati Timu toka nchi 41 ndio zinashiriki Confederation Cup bila uwepo wa nchi 4 nazo ni Cameroon, Malawi, Gabon na Namibia.
CAF CHAMPIONS LEAGUE 2023-2024 Tanzania tunawakilishwa na Yanga na Simba na katika Utaratibu wa kuanza Mashindano lazima kuwepo na droo ili kupata mpangilio wa kuweza Timu zote kushiriki na kupata Timu 16 za kuingia Group Stage.
Msimu huu Kutokana na Timu 8 zinazoshiriki African Super League kutakiwa kuanza 2nd Preminary Round ambayo ni hatua ya mwisho kwenda Group Stage na pia Idadi ya timu shiriki kuwa 54 kwa mujibu wa kikokotoo cha CAF basi unachukua Timu shiriki 54.
Timu hitajishi 32 = 22 ambayo hii ndio michezo inayopaswa kuchezwa mwanzoni sawa na Timu 44, Unachukua Timu shiriki 54 - Idadi ya timu za kucheza Mwanzo 44 = Timu zitazoanza 2nd Preminary 10.
(54-32)×2 = 44 54-44 = 10
Kutokana na Idadi inayopaswa kuwa Timu 10 ndio zinakwenda kuanza 2nd Preminary kuanza 15-27 September 2023 na Timu 44 kuanzia 1st Preminary ambazo zitachezwa 18-27 August 2023 na kufanya Timu 22 zitazoshinda kwanza zitaungana na Timu 10 kufanya Jumla ya timu 32 ambazo zitagombania Kupata Timu 16 za Kuingia Group Stage.
Hivyo Basi Timu 8 za African Super League ambazo ni Al Alhy, Wydad, Esperance, Mamelod, Simba, Petro de Luanda, TP Mazembe na Enyimba zinaungana na Timu 2 za CR Belouizdad na Pyramid kufanya jumla ya Timu 10 zinazoanzia 2nd Preminary Round na Timu zingine 44 zilizosalia zitaanzia mwanzoni ikiwemo Yanga ya Tanzania.