Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vilabu EPL vyakubaliana Mikataba mwisho miaka mitano

Enzo Record.jpeg Kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vilabu vya Ligi Kuu England (EPL) zimepiga kura ya kupitisha Sheria ya mwisho wa ukomo wa mikataba ya wachezaji watakaosajiliwa katika madirisha ya usajili au kuongezewa mkataba akiwa anaendelea kuitumikia timu yake husika.

Vilabu vimefikia muafaka kuwa ukomo wa mikataba uwe muda wa miaka 5 tu na sio zaidi ya hapo. Hivyo hakuna timu itakayoruhusiwa kumpatia mchezaji mkataba wenye urefu wa zaidi ya miaka 5.

Kufuatia hatua hiyo vilabu vya ligi kuu ya England sasa vitaendana na kanuni za UEFA ambazo zilibadilishwa majira ya joto

Aidha hatua hiyo ni pigo kwa vilabu kama Chelsea ambayo ilitumia mbinu ya kuwapa wachezaji mkataba mrefu ili kujaribu kuepuka rungu la sheria ya za kifedha za UEFA (FFP).

Mbinu ya kuwasainisha wachezaji mikataba ya muda mrefu imekuwa ikizisaidia timu kugawanya gharama kubwa za wachezaji wanaowasajili hatua kwa hatua kulingana na urefu wa mikataba yao Chelsea ikifanya hivyo kufuatia usajili wa wachezaji kama vile Enzo Fernández, Mykhailo Mudryk na Moisés Caicedo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live