Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vilabu EPL kupiga kura ya kufuta matumizi ya ‘VAR’

Sdv Var Vilabu EPL kupiga kura ya kufuta matumizi ya ‘VAR’

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu zinazoshiriki Premier League zimeombwa kuunga mkono hoja iliyowasilishwa na Klabu ya Wolverhampton Wanderers inayopendekeza azimio la kupiga Kura ya kufuta Matumizi ya ‘VAR’ kuanzia Msimu ujao.

Pendekezo hilo ambalo linadaiwa kupingwa na Bodi ya Ligi Kuu linatarajiwa kusikilizwa Juni 6, 2024 ambapo imeelezwa Bodi inatambua haki ya Wolves kutoa pendekezo hilo, lakini inadhani kufutwa kwa #VAR kunaweza kusababisha maamuzi mengi yasiyo sahihi.

Aidha, baadhi ya Maafisa wa EPL wanadai pendekezo hilo litaathiri Ubora wa Ligi, pia kwa mujibu wa takwimu za Msimu huu zinaonesha kiwango cha maamuzi sahihi ya Uwanjani kimeongezeka kutoka 82% hadi 96 kupitia VAR.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live