Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikwazo kwa Taifa Stars kuifikia Qatar 2022

Staars Kikosi Kikosi cha Timu ya Taifa

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taifa Stars inaongoza katika msimamo wa Kundi J, wakiwa na pointi nne (4) baada ya jana kuibuka na ushindi dhidi ya timu ngumu ya Madagascar katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Wengi wamefurahi na kuisifu Stars kwa kiwango bora ilichoonesha katika mchezo huo bila kujua ni hatua zipi ambazo Stars kama atafanikiwa kuibuka kinara atahitajika apite ili aweze kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kule Qatar 2022.

Mosi, hatua ambayo Stars ipo hivi inajumuisha timu 40 ambazo zimewekwa katika makundi 10, ili kwenda hatua inayofuata unahitaji uongoze kundi ulilopo baada ya kukamilika kwa michezo 6 ambayo kila timu inapaswa kucheza.

Pili, Vinara wa kila kundi watakapopatikana zitapatikana timu kumi ambazo zitapangwa baina yao na watacheza michezo miwili nyumbani na ugenini, na washindi kutoka katika mechi hizo watakwenda Qatar.

Mpaka kufikia hapo zitapatikana timu 5 zitakazoiwakilisha Afrika katika Mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

Kwa maana hiyo Stars anapaswa kufanya vizuri dhidi ya Benin na DR Congo ili apate nafasi ya kuliongoza kundi alilopo.

Atakapopita basi itakua ni mtihani mwingine kwake kwenda kushindana na wale vigogo tisa (9) walioongoza katika makundi yao.

Msimamo wa kundi J

Chanzo: www.tanzaniaweb.live