Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana wa Gamondi walichagua kumheshimu mzee Kibadeni

Kibaden Maxiii Vijana wa Gamondi walimheshimu mzee Kibadeni

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rekodi ya King Kibadeni ilikua ivunjwe rasmi jana na Max Nzengeli lakini nilichokiona kwa wachezaji wa Young Africans Sports Club ni kutokua na ubinafsi moyoni, Max angeweza kupiga yeye penati lakini akamuachia Pacome apige, Aziz Ki angeweza kupiga yeye akaacha Pacome apige.

Clement Mzize kijana mdogo ndani ya safu ya ushambuliaji ya Yanga Sc alimpima Mohaned Hussein akaingia hatimae akaingia kwenye mfumo.

Nyota wa matokeo ya Yanga ni Diarra alipomaliza kazi kwa mgeni wa Simba Sc bwana Kibu Denis mkandaji ambapo pia unaweza sema mgeni mkandamizwaji, kutoka kwake liligeuka pigo kubwa.

Niliwahi kusema ukuta wa Simba Sc unapwaya sana ikitokea wakakutana na timu yenye uchu na hasira itakua dhahama wapo waliopinga kwa mahaba tu binafsi na sio hoja ya kisoka.

Mpaka sasa Simba Sports Club imefunga mabao kumi na Saba lakini imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara kumi kitu ambacho kwa miaka ya hivi karibuni hakikutokea kwa Simba Sc, kuruhusu mabao kumi ndani ya mechi Saba tu ni dhahiri wana kazi ngumu ya kufanya hii ni rekodi mpya kwao.

Simba Sports Club ilikua ianze kufungwa na Yanga kule TANGA lakini aina ya uchezaji ulifanya mechi ile iende kwenye matuta, hawakucheza kama wakubwa siku ile lakini jana wakacheza kikubwa yaani njoo na mimi nije, tupashane kwenye msitari hapo kati yaliyotokea ndio yale.

Kauli ya mashabiki tunashinda lakini hatuna furaha ilikua ikizodolewa na msemaji Ahmed Ally lakini hata yeye jana amekimbia waandishi haraka sana yaani alichokifanya Popat nae kafanya. Kuna muda jicho la shabiki huwa linaona sana licha ya kutokua na leseni ya ukocha.

Kwa timu zote mbili Yanga Sc walikua wanapitika sana kushoto kirahisi hasa kipindi cha kwanza baadae wakakaa sawa, Simba walikua wanapitika sana kirahisi kushoto pia. Kiufupi upande wa kushoto kwa timu zote jana ndio ulikua mwepesi zaidi kupita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live