Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viingilio Yanga vs CR Belouizdad

CR Belozdad V Yanga Viingilio Yanga vs CR Belouizdad

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viingilio vya mchezo wetu ujao wa kimataifa kati ya Yanga dhidi ya CR Belouizdad utakaochezwa Februari 24, 2024, vimetajwa.

Mchezo huo wa Kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika, umepangwa kuchezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Katika viingilio hivyo, kuna makundi manne, V.I.P A Tsh 30,000, V.I.P B Tsh 20,000, V.I.P C Tsh 10,000 na Mzunguko Tsh 5,000.

Huu ni mchezo muhimu kushinda, hivyo Mwananchi fanya haraka kupata tiketi yako na uje uwanjani mapema kuwapa sapoti wanajeshi wetu watakapokuwa wanaipambania nembo ya klabu.

Ukiangalia msimamo wa Kundi D, timu ya Young Africans SC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano sawa na CR Belouizdad, hivyo ushindi utawapa mwanga wa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: