Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo wazidi kuongezeka mbio za saini ya Joao Neves

Fvds Neves Joao Neves

Fri, 14 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Liverpool inataka kuwasilisha ofa kwenda Benfica kwa ajili ya kuipiku Manchester United na kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo ya Ureno, Joao Neves katika dirisha hili.

Taarifa zinaeleza, mabosi wa Liverpool wanataka kutumia uhusiano mzuri walionao na Benfica kuhakikisha wanakamilisha dili hilo.

Liverpool ilijenga uhusiano na Benfica wakati wa usajili wa Darwin Nunez mwaka 2022 ambapo kwa sababu hiyo wanaamini itakuwa ni rahisi pia kufanya biashara ya kumchukua Neves.

Staa huyu wa kimataifa wa Ureno amekuwa akigombaniwa na vigogo wengi kutoka England ambapo mbali ya Man United na Liverpool, matajiri Man City pia wanahusishwa kutaka kumsajili.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, katika mkataba wa Neves kuna kipengele ambacho kinairuhusu timu inayomhitaji kutoa Euro 120 milioni ili kuuvunja na kuipata huduma yake.

Timu nyingi zinaonekana kuwa hazipo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa na badala yake zinajaribu kufanya mazungumzo na Benfica ili kumnunua kwa bei ya chini kiungo huyo kinda mwenye umri wa miaka 19 mwenye kipaji.

Chanzo: Mwanaspoti