Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo waweka turufu yao kwa Yanga

Bangala, Mayele Tunis.jpeg Nyota wa Yanga wakiwa mazoezini nchini Tunisia

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga iko nchini Tunisia na leo itacheza mchezo wa kwanza wa makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir, huku mmoja wa vigogo wa timu hiyo akiweka turufu yake kwa vinara hao wa Ligi Kuu bara ikitoboa na kurejea nchini kwa ushindi mtamu.

Wawakilishi hao wa Tanzania watavaana na Watunisia kwenye Uwanja wa Stade Mustapha Ben Jannet na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Seif Gulamali aliliambia Mwanaspoti kwa maandalizi waliyofanya na morali waliyonayo wachezaji pamoja na maandalizi makubwa yaliyofanywa na viongozi ana imani kubwa kuwa watashinda mchezo huo.

Gulamali, aliye pia Mbunge wa Manonga,Tabora ndiye mkuu wa msafara wa timu hiyo iliyopo Tunisia akizungumza kwa njia ya simu kutoka Tunis, alisema licha ya hali ya hewa kuwa ya baridi kali, lakini wachezaji wameanza kuzoea na wana imani hadi kufikia siku ya mchezo (kesho) watakuwa fiti na kukiwasha uwanjani bila wasiwasi wowote.

“Wachezaji wana ari kubwa kuhakikisha kwamba wanapata ushindi na tumejiandaa kuhakikisha kwamba tunafuzu hatua hii ya makundi na kwenda robo fainali timu iko vizuri. Morali ya wachezaji iko vizuri sana wanataka kuonyesha vipaji vyao na waonekane nje ya Afrika hasa ukizingatia Timu inafuatiliwa katika kipindi hiki cha mashindano,” alisema Gulamali.

Chanzo: Mwanaspoti