Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo wategeana uchaguzi Simba

Murtaza Mqngunguuu.jpeg Vigogo wategeana uchaguzi Simba

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kamati ya Uchaguzi wa Simba ilifungua mlango kwa wagombea kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali tangu Desemba 5, mwaka huu lakini hadi jana Jumamosi hakuna mgombea aliyejitokeza kuchukua ya uenyekiti.

Nafasi ya mwenyekiti ambayo inawaniwa ipo chini ya Murtaza Magungu ambaye alichaguliwa kwenye uchaguzi mdogo baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi kujiuzuru.

Ni wajumbe wanne pekee wamechukua fomu hizo ambao ni Abubakari Zebo aliyechukua Desemba 6, Abdallah Rashi Mgomba, Hawa Mwaifunga na Iddy Noor Kajuna waliochukua Desemba 7.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Boniface Lihamwike aliliambia Mwanaspoti kuwa bado kuna muda kwa wenye nia ya kuwania nafasi hizo kwani mwisho ni Desemba 19.

Simba wanafanya uchaguzi huo baada ya viongozi waliopo madaraka kuongoza kwa miaka minne kwa mujibu wa katiba. Nafasi zinazowaniwa ni mwenyekiti na wajumbe wanne pekee.

Kwa mujibu wa katiba yao, mwenyekiti atakayechaguliwa ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili ambao wataingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi wakitimiza idadi ya wajumbe saba kutoka upande wa klabu kuingia katika bodi hiyo.

“Hakuna aliyechukua fomu upande wa mwenyekiti hadi sasa. Majina niliyonayo ni hayo manne ambao ni Kajuna, Mgomba, Hawa na Zebo, naamini wataendelee kujitokeza kwani muda upo,” alisema Lihamwike ambaye ni Hakimu Mkazi wa Kiteto mkoani Manyara.

Chanzo: Mwanaspoti