Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo Uturuki waanza kumnyatia Greenwood

Greenwoodz Mason Greenwood

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Fenerbanhce imepanga kuingia kwenye vita ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Manchester United, Mason Greenwood, 22, katika dirisha hili ikiwa ni moja kati ya timu zilizovutiwa na kiwango alichoonyesha msimu uliomalizika alipokuwa akicheza kwa mkopo Getafe.

Inaelezwa moja kati ya sababu zinazoifanya Fenerbanhce ihitaji kumsajili staa huyu ni maelekezo kutoka kwa Jose Mourinho anayetarajiwa kuwa kocha wao mpya kwa msimu ujao.

Man United haina mpango wa kumrudisha Greenwood kikosini licha ya kuonyesha kiwango bora akiwa na Getafe kwa sababu wachezaji wa timu ya wanawake na baadhi ya wafanyakazi wanapinga suala hilo wakidai kwamba wanahofia usalama kutokana na kitendo cha mshambuliaji huyo kutuhumiwa kumfanyia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia mzazi mwenzie ingawa hakukutwa na hatia.

Huduma ya Greenwood pia inahitajika na baadhi ya timu nyingine barani Ulaya ikiwemo Juventus.Mkataba wake unaisha mwakani.

Chanzo: Mwanaspoti