Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo Ulaya wamiminika kwa Rabiot

Rabbiot 2024 Vigogo Ulaya wamiminika kwa Rabiot

Sat, 3 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal, Real Madrid na Atletico Madrid zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa zamani wa Juventus na Italia, Adrien Rabiot, ambaye kwa sasa yupo huru baada ya mkataba wake na Juve kumalizika katika dirisha hili.

Awali Rabiot alidaiwa kuwa katika hatuya za mwisho kujiunga na Man United na Liverpool lakini hadi sasa hajakamilisha uhamisho wa timu yoyote kati ya hizo.

Timu nyingi zimevutiwa na fundi huyu wa kimataifa wa Ufaransa kutokana na kiwango bora alichoonyesha mwaka huu katika michuano ya Euro, pia kuwa kwake huru.

Rabito ambaye msimu uliopita alicheza mechi 35 za michuano yote na kufunga mabao matano.

Kiungo huyu alikuwa akihusishwa kuondoka Juventus tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi na timu iliyoonekana kuwa karibu kumpata ilikuwa ni Man United lakini dili lilifeli dakika za mwisho na akasaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuwepo Juve ambao umemalizika katika dirisha hili.

Crysencio Summerville

KWA mujibu wa tovuti ya Skysports, West Ham ipo katika hatua za mwisho kusajili washambuliaji wawili katika dirisha hili wakwanza ikiwa ni straika wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Niclas Fullkrug, 31, na wapili ni mshambuliaji wa Leeds na Uholanzi, Crysencio Summerville, 22. Mabosi wa Leeds wanahitaji saini ya fundi huyu kwa ajili ya kuboresha zaidi eneo lao la ushambiliaji.

Romelu Lukaku

ASTON Villa imeripotiwa kufanya makubaliano na Chelsea juu ya usajili wa Romelu Lukaku katika dirisha hili lakini staa huyo amekataa kujiunga nao na badala yake amawaambia kwamba anataka kutua Napoli ili kuungana na kocha wake wa zamani, Antonio Conte. Villa ilikuwa ikihitaji huduma ya Lukaku katika dirisha hili baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha.

Aaron Wan-Bissaka

MABOSI wa West Ham wameshafikia makubaliano na beki wa kulia wa Manchester United, Aaron Wan-Bissaka, 26, na wanataka kumsajili katika dirisha hili lakini hadi sasa hawajafikia muafaka na Man United kwenye masuala ya ada ya uhamisho. Man United inahitaji Pauni 18 milioni ili kumuuza Bissaka wakati West Ham ikiwa tayari kutoa Pauni 10 milioni pekee.

Jorge Cuenca

FULHAM ipo katika mazungumzo na Villarreal ili kuipata saini ya beki wa kati wa timu hiyo na Hispania Jorge Cuenca, katika dili ambalo linaweza kuigharimu kiasi cha Pauni 6.7 milioni. Cuenca mwenye umri wa miaka 24, amevutia vigogo wengi Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha kwa msimu uliopita ambapo alicheza mechi 37 za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwakani.

Billy Gilmour

NAPOLI imewasilisha ofa ya Pauni 10.2 milioni kwenda Brighton kwa ajili ya kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo na Scotland, Billy Gilmour katika dirisha hili ambayo inadaiwa kukubaliwa. Hata hivyo, kabla ya kukamilisha usajili wake Napoli inataka kuuza baadhi ya wachezaji ikiwemo Victor Osimhen. Mkataba wa Gilmour unamalizika 2026.

Mikel Moreno

ARSENAL ipo katika hatua za mwisho kufikia muafaka na Real Sociedad juu ya usajili wa kiungo wa timu hiyo na Hispania, Mikel Moreno, 28, katika dirisha hili.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Mirror, dili hilo linaweza kukamilika kwa kiasi cha pesa kinachofikia Pauni 25 kilioni. Moreno mwenyewe alishakubali kutua kwa washika mitutu hao muda mrefu na kinachochelewesha dili ni makubaliano baina ya timu juu ya ada ya uhamisho.

Tammy Abraham

ROMA imeshaanza kutafuta mbadala wa Tammy Abraham anayedaiwa kuwa katika mchakato wa kutua AC Milan na taarifa kutoka tovuti ya The Repubblica zinadai wameshafikia muafaka wa kumsajili straika wa Girona na Ukraine, Artem Dovbyk, 27, katika dirisha hili kwa ada ya uhamisho ya Pauni 28.8 milioni. Artem mwenye umri wa miaka 27, msimu uliopita alicheza mechi 12 za michuano yote na kufunga bao moja. Mkataba wake unamalizika 2026.

Chanzo: Mwanaspoti