Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo Qatar wawasilisha ofa rasmi kuinununa Man United

Ofa Man United Vigogo Qatar wawasilisha ofa rasmi kuinununa Man United

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwekezaji kutoka Qatar, Sheikh Jassim Bin Hamad Al Thani, ambaye ni Mwenyekiti wa benki moja ya Qatar QIB amewasilisha ofa ya Euro bilioni 5 kwa ajili ya kuinunua klabu ya Manchester United.

Akithibitisha kuwasilisha ofa hiyo Al Thani ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Qatari, Hamad bin Jassim bin Jaber Al Thani amesema zabuni hiyo inapanga kurejesha klabu katika hadhi yake ya zamani ndani na nje ya uwanja. Zaidi inalenga kuwaweka mashabiki kwenye moyo wa Manchester United.

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha zabuni ya kununua klabu hiyo ni Ijumaa Februari 17 majira ya saa 10 Usiku kwa muda wa UK sawa na saa 7 usiku siku ya Jumamosi kwa saa za Afrika Mashariki. Muda huo umepangwa na Benki ya Reine Group iliyopewa jukumu la kusimamia uuzwaji wa Mashetani hao Wekundu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live