Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo Man United wapagawana na Osimhen

Victor Osimhen.jpeg Victor Osimhen

Sun, 28 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kauli ya rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis kwamba straika wa timu hiyo, Victor Osimhen anaweza akaondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi inadaiwa kuwashawishi vigogo wa Manchester United.

Vigogo hao wa Masherani Wekundu wanatarajiwa kutuma ofa mwishoni mwa msimu kwa ajili ya kutaka kumsajili Osimhen ikiaminika kwamba huenda akasaidia kuondoa upungufu uliopo kwenye eneo la ushambuliaji.

Licha ya kusajiliwa Rasmus Hojlund katika dirisha lililopita Man United bado imekuwa ikisumbuka na ubora wa eneo lao la ushambuliaji.

Uamuzi wa Osimhen kuondoka unadaiwa kufanywa tangu mwaka jana na mbali ya Man United PSG imekuwa ilitajwa sana kutaka kumsajili ili akazibe pengo la Kylian Mbappe ikiwa ataondoka.

Napoli iko tayari kumuuza kwa zaidi ya Euro 150 milioni Osimhen ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 25.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live