Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo Chelsea kutembelea Tanzania Jumatano

Chelsea Jumatano Vigogo Chelsea kutembelea Tanzania Jumatano

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baadhi ya wawakilishi wa timu ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu nchini England wanatarajiwa kuwasili Tanzania Jumatano kwa ajili ya kukutana na viongozi wa serikali ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa mujibu wa mratibu wa Chelsea hapa nchini, Mohamed Reza Saboor amesema msafara huo utawajumuisha meneja wa biashara, Carly Telford na Barnes Hempel, ambaye ni mkuu wa kitengo cha uuzaji.

Ameongeza kuwa lengo la msafara huo ni kusaini makubaliano ya kutangaza masuala ya utalii na michezo hapa nchini.

Saboor amesema vigogo hao watakutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi pia watakutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar Tabia Maulid Mwita.

Hata hivyo watafika Tanzania Bara kukutana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro ambapo watajadili baadhi ya mambo kuhusiana na maendeleo ya michezo nchini.

Chanzo: Mwanaspoti