Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo Barca watuma salamu kwa Kante

Kante Pic Ngolo Ngolo Kante

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kuna uwezekano Barcelona ikatuma ofa kwenda Chelsea ili kuipata huduma ya kiungo wa timu hiyo, N’Golo Kante katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa mkataba wake na Chelsea unatarajiwa kumalizika na Barca inamhitaji ili akawe mbadala wa kiungo Mhispania, Sergio Busquets, 34, ambaye kuna uwezekano akaondoka mwishoni mwa msimu huu.

Busquets anataka kuondoka Barca ili kutafuta changamoto mpya na timu ambazo amekuwa akihusishwa nazo kwa sasa ni Inter Miami ya Marekani.

N’golo ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kuondoka Chelsea kwa sababu timu hiyo haitaki kumpa ofa ya mshahara sahihi anaouhitaji na kufuatia hatua hiyo Chelsea imeshaanza kuangalia uwezekano wa kuachana nyota huyo.

Chanzo: Mwanaspoti