Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vieira: Zaha haondoki Crystal Palace

Wilfred Zaha X Vieira Wilfred Zaha na Kocha wa Palace Patrick Vieira

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya Crystal Palace Patrick Vieira amesema kuwa mchezaji wake anayecheza katika timu ya Taifa ya Ivory Coast na timu ya Crystal Palace haendi popote atabaki kukitumikia kikosi hicho baada ya dirisha hili la usajili.

Vieira amesema;

"Ninafanya kazi naye kila siku na hakuna kitu kitaingia akilini mwangu kwamba kitu kama (Zaha kuondoka kitatokea)"

Hakuishia hapo pia aliongeza kwa kusema kuwa kitu pekee anachoonyesha ni ushindani uwanjani, kufanya vizuri kwa klabu hii ya soka ambayo anaipenda sana. Patrick Vieira ambaye ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu aliichukua timu hii msimu jana ambayo ilikuwa chini ya kocha mkuu Roy Hodgson.

Willfred Zaha ambaye ni nyota wa timu hiyo amekuwa na kiwango kizuri sana msimu huu hivyo kufanya kuwa na tetesi za yeye kutakiwa na timu mbalimbali ikiwepo Chelsea. Zaha amekuwa akitoa mchango mkubwa sana katika timu yake hata ujio wa Vieira umemfanya aimarike lakini pia takribani kikosi kizima kimekuwa na ubora mzuri ambao unaleta ushindani kwa vilabu vikubwa na hata vilabu vya madaraja yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live