Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Victor Osimhen aipeleka Napoli Robo Fainali

Victor Osimhen Two Goals.jpeg Victor Osimhen

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Victor Osimhen amefunga magoli 24 katika mechi 28 za mashindano yote ya Napoli msimu huu ukiwa ni msimu bora kabisa kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria.

Ametimiza mabao hayo kwa kuifungia Napoli bao mbili kwenye ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa dimba la Diego Maradona Jumatano.

Matokeo hayo yanaifanya Napoli kufuzu kucheza robo fainali kwa jumla ya bao 5-0 baada ya raundi ya kwanza Napoli ya kocha Luciano Spalletti kushinda bao 2-0.

“Tuendelee kufurahia mpira na kuangalia mbele yetu kuhakikisha kuna rekodi ambayo tunaiacha hapa klabuni”, alisema Osimhen ambaye bao moja alifunga kwa kichwa lingine ni kuugusa.

Bao la tatu kwa Napoli lilikuwa la mkwaju wa penati kupitia kwa Piotr Zielinski likifungwa dakika ya 64.

Itajua itacheza na nani hatua ya robo fainali kupitia droo ambayo itafanyika Ijumaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live