Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vichaka vitano vya Ronaldo ikifika Januari

Ronaldo UEFA Cristiano Ronaldo

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa, Cristiano Ronaldo hana muda mrefu wa kuagana na Manchester United kama kocha Erik ten Hag ataamua kumfungulia mlango wa kutokea wakati wa usajili wa dirisha la Januari.

Ronaldo alirejea Man United na kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Juventus, lakini sasa tayari ameshaanza mipango ya kuachana na maisha ya Old Trafford. Wakati Ronaldo akihusishwa na mpango wa kuondoka Man United, maswali yanayoulizwa mkali huyo wa kimataifa wa Ureno atakwenda wapi? Hizi hapa timu tano ambazo Ronaldo anaweza kwenda kumalizia soka lake.

-Sporting Lisbon. Kwenye kikosi hicho, Ronaldo atarudi nyumbani alikoanzia maisha yake ya soka na mama yake mzazi anachotaka ni kumwona mwanaye anarudi kukipiga katika timu hiyo ya utotoni.

-Real Madrid. Hii ni timu nyingine aliyowahi kuichezea Ronaldo na kuandika rekodi kubwa ikiwamo ya kufunga mabao 450. Hata hivyo, haionekani kama kocha Carlo Ancelotti atahitaji saini ya mchezaji huyo kwenye kikosi chake kwa sasa.

-Chelsea. Kwenye dirisha lililopita, Ronaldo alihusishwa sana mpango wa kutua Stamford Bridge. Mmiliki mpya wa Chelsea, bilionea Todd Boehly anaripotiwa kuwa shabiki mkubwa wa Ronaldo na huenda akamvuta akakipige kwenye kikosi cha The Blues.

-Saudi Arabia. Chaguo jingine ambalo Ronaldo anaweza kufanya ni kufunga pazia lake kwenye soka la Ulaya na kwenda kukipiga kwenye ligi ya Saudi Arabia. Klabu ya Al-Hilal iliripotiwa kumtengea Ronaldo Pauni 210 milioni kwa mwaka akajiunge kwao.

-Qatar. Mahali kwingine kwenye timu zenye pesa ya kumudu gharama za Ronaldo ni za Qatar. Staa huyo bila ya shaka anaweza kuvutiwa kwenda kumalizia soka lake Qatar, mahali ambako atapata pia fursa ya kufanya utalii na familia yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live