Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Veterans Middle Age yapeleka moto mabingwa wa mikoa

Fcxtafs Veterans Middle Age yapeleka moto mabingwa wa mikoa

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mabingwa wa Ligi ya Mkoa wa Tanga, Veterans Middle Age inaonekana wamepania msimu huu baada ya kocha Masoud Magendo kueleza kwa msisitizo kuwa wanakwenda kumalizia hatua waliyobakisha mara ya mwisho waliposhiriki Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2021/2022.

Katika msimu huo, Veterans walipania kupanda First League, lakini hawakufanikiwa, lakini sasa wameapa kuwa iwe mvua au jua msimu huu wanaitaka ligi hiyo.

Veterans ambao wamepangwa kundi C katika kituo cha Manyara watachuana na timu za Raggae boys ambao ndio wenyeji, Arusha City (mabingwa wa Mkoa wa Arusha), Kawele FC kutoka Kilimanjaro, Mabao ya Shinyanga, Maswa FC kutoka Simiyu pamoja na Eagle ambao ni mabingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Timu hiyo ambayo mara ya mwisho ilikwenda kuuwakilisha Mkoa wa Tanga kwenye michuno ya RCL msimu wa 2021/2022, ilimaliza nafasi ya tatu katika kundi lake nyuma ya TMA na TRA mkoani Kilimanjaro na sasa wanakwenda kutupa karata kwa mara nyingine.

Akizungumza, kocha wa Veterans Middle Age, Masoud Magendo amesema wachezaji ambao walishiriki 2021/2022 walikuwa bado vijana wadogo, hivyo walishindwa kuhimili mikiki licha ya kushika nafasi ya tatu kwenye kundi.

"Mara ya mwisho kushiriki tulikwenda na vijana wengi wakiwa ni wadogo na ni mara ya kwanza kushiriki mashindano yale, lakini sasa wale wote tuliokuwa nao wapo na utimamu, wanajua vizuri michuano hii. Mashindao yanajulikana ni magumu msimu huu tumejipanga zaidi kwenda kushindana," amesema Masoud.

Hata hivyo amesema kwa sasa anaamini msimu huu hawatakwenda kinyonge na timu walizopangiwa nazo ana uhakika wanazimudu kwani amefanya maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha lengo la kutwaa ubingwa inatimia.

"Tumecheza mechi nyingi za kirafiki kwa ajili ya kuwaweka wachezaji wetu mguu sawa kwenye michuano ya msimu huu. Nashukuru timu iko vizuri, tumefanya maandalizi yote muhimu," amesema.

Amesema wakati michuano hiyo ikitarajiwa kuanza Machi 8, Veterans Middle Age itaondoka Tanga siku nne kabla na kikosi cha wachezaji 25 ili kuwahi kuzoea mazingira.

Mkurugenzi wa timu hiyo, Halid Abdallah amesema wamefanya maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha kuwa hakutakuwepo na changamoto zitakazojitokeza na wapo tayari kwa mapambano.

"Timu itasafiri kwenda Manyara kikubwa mpira una matayarisho yake na sisi sio wageni kwenye mpira, lakini kama kuna mtu anatamani kuyusaidia tunamkaribisha wala hatumzuii," amesema.

Ameongeza kuwa, " tuko tofauti na timu nyingine. Kazi yetu kubwa hasa ni kuzalisha vipaji na ndio maana tunachukua vijana wadogo na hiyo ndiyo falsafa yetu. Ukitaka kuingia kwenye mpira lazima ukubali kupoteza muda mwingi na pesa. Mafanikio yanakuja baadaye sana, vinginevyo utaishia njiani."

Abdallah amesema: "Tumeshatoa vijana wengi hivi sasa wapo kwenye timu zikiwemo Coastal Union, African Sports za Tanga na mikoani wapo waliowahi kuzichezea timu za vijana za Simba Yanga na Kagera. Kwa hiyo ni jambo la kujivunia kwetu kama wadau wa soka."

Chanzo: Mwanaspoti