Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vardy nje wiki nne

Vardyy Jamie Vardy atakosekana kwa takribani wiki nne

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa kati wa Leicester City Jamie Vardy atakuwa nje ya uwanja kutokana na majeruhi kwa takribani mwezi mmoja baada ya kupata mshikeli kwenye mtanange wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool uliomalizika kwa faida yao.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, alifanyiwa huduma ya kwanza uwanjani kwenye mechi hiyo baada ya kugongana na mlinzi wa Liverpool Joel Matip ingawa alilazimika kucheza mpaka kipenga cha mwisho cha mwamuzi, itakumbukwa pia Disemba 26 alikosa mechi dhidi ya Manchester City kwa majeruhi sawa na ya sasa.

“Tunaweza kumkosa kwa wiki tatu au nne zijazo”, alisema kocha Brendan Rodgers.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live