Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Varane kurudi Real Madrid

Varane Azima Tetesi Za Kuhamia Saudia Rafael Varane

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Klabu ya Real Madrid huenda ikajaribu kumsajili tena beki wao wa zamani ambaye kwa sasa anaichezea Manchester United, Raphael Varane, baada ya beki wao kutoka Austria, David Alaba, 31, kupata majeraha ambayo yanatarajiwa kumuweka nje kwa muda mrefu.

Hata hivyo, inaonekana kutakuwa na ugumu kwenye kumpata kwenye dirisha hili kwa sababu kocha wa Mashetani Wekundu hao hayuko tayari kumuachia kwa sasa.

Varane mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na Man United mwaka 2021, msimu huu amecheza mechi 14 za michuano yote na mkataba wake wa sasa unamalizika msimu ujao.

Awali, Beki huyo kutoka Ufaransa alikuwa anahusishwa kuwa kwenye rada za baadhi ya vigogo kutoka Saudi Arabia ambao walimhitaji tangu dirisha lililopita.

Ilidaiwa kuwa kocha wa Erik ten Hag hakuwa na uhusiano mzuri na staa huyu hadi akawa anamuweka benchi kwenye mechi kadhaa zilizopita lakini kwa sasa wanadaiwa kuyamaliza na kila kitu kipo sawa.

Chanzo: Dar24