Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Varane amfuata de Gea

Varane Pic Varane amfuata de Gea

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ikiwa ni saa kadhaa baada ya kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kitakachochujwa kwa ajili ya Kombe la Dunia kutoka bila jina la David de Gea, staa mwingine wa Manachester United, Raphael Varane huenda asiwepo kwenye mashindano hayo baada ya kocha wake wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps kuthibitisha hilo.

Deschamps amesisitiza hatachagua mchezaji yeyote ambaye atakuwa na majeraha, hivyo wote wanaoujiuguza hawatakwenda Qatar.

Varane kwa sasa anauguza majeraha aliyopata kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Majeraha hayo yanadaiwa kuwa huenda yatamuweka nje kwa kipindi kisichopungua mwezi mmoja ambapo anakadiriwa kuwa huenda akawa amepona siku za mwisho za maandalizi ya Kombe la Dunia.

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag alithibitisha kuwa staa huyo hatakuwepo kwenye mechi zote hadi pale ligi itakaposimama kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Dunia.

“Varane hayupo kwenye kikosi, hatacheza nafikiri hadi Kombe la Dunia litakapoanza,” alisema Ten Hag. Matumaini ya mashabiki wengi ni kuwa beki huyo huenda angejumuishwa kwenye kikosi.

“Ni wazi kwamba nilisema hapo awali siwezi kumchukua mchezaji yeyote majeruhi kwenye mashindano makubwa kama haya. Siwezi kumchukua mchezaji ambaye hatacheza mwanzoni mwa mashindano,” alikaririwa Descamps akisema.

Varane anakuwa mmoja kati ya wachezaji wengi wa Ufaransa ambao watakosekana kwenye Kombe la Duniani akiungana na Paul Pogba, Lucas Digne, Lucas Hernandez na N’Golo Kante.

Fainali za Kombe la Dunia zinatarajiwa kuanza Novemba mwaka huu.

Chanzo: Mwanaspoti