Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Varane afunguka kilichomuondoa Timu ya Taifa ya Ufaransa

Raphael Varane Rapahael Varane alitangaza kuachana na Timu ya Taifa ya Ufaransa

Sun, 5 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raphael Varane amefichua sababu iliyomfanya kustaafu mapema kuichezea Ufaransa, akisema kwamba alikuwa akipambana na ratiba ya michezo kubana.

Varane alitanga kuacha kuichezea Ufaransa Kimataifa Alhamis ya Tarehe 2/2/2023, baada ya kumalizika kwa kombe la dunia 2022 licha ya kuonekana kuwa katika kilele chake na akiwa bado miezi miwili kabla ya kutimiza miaka 30.

Hatimaye beki huyo wa Manchester United amefunguka jinsi alivyolazimika kucheza mara kwa mara katika kiwango cha juu kumemletea madhara na kupelekea kuchukua uamuzi mgumu wa kuacha kuichezea Ufaransa.

“Tuna ratiba zilizobana kupita kiasi na tunacheza bila kukoma, Hivi sasa ninahisi kama ninakosa pumzi ninapokutana na mchezaji msumbufu”

Tangazo la Varane lilikuwa la mshtuko zaidi ikizingatiwa alionekana kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa nahodha ajaye wa Ufaransa baada ya Hugo Lloris kuthibitisha kustaafu kwake kimataifa mwezi uliopita.

Varane aliichezea nchi yake mechi 93 tangu acheze mechi yake ya kwanza mwaka 2013, na alikuwa mhimili mkuu wa safu ya ulinzi kwa muongo mmoja.

Alicheza kila dakika kwenye Kombe la Dunia la 2018 huku Les Bleus wakinyanyua kombe hilo kwa mara ya pili katika historia yao, na alichukua jukumu muhimu katika mbio za Ufaransa hadi fainali huko Qatar mwaka jana.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 pia alishinda Ligi ya Mataifa na nchi yake mnamo 2021, wakati Ufaransa ilitoka nyuma na kuifunga Uhispania 2-1 kwenye fainali.

Hakufanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ulaya (Euro), kwani Ufaransa ilifuzu katika fainali ya 2016 dhidi ya Ureno, na huenda kukawa na kishawishi cha kuendelea kucheza hadi mashindano ya mwakani.

Lakini amechagua kuachana na soka la kimataifa baada ya kukiri kuwa lilikuwa na athari kwa ustawi wake wa kiakili.

Kustaafu kwa Varane kulikuja kuwashangaza wengi, lakini kulikubaliwa kabisa na meneja wa Ufaransa Didier Deschamps, ambaye alimshukuru beki huyo wa kati kwa kujitolea kwake bila kuyumba kwenye jezi ya Ufaransa.

Varane ni mchezaji wa tatu wa Ufaransa mwenye hadhi ya juu kustaafu kucheza kimataifa katika kipindi cha wiki chache, akifuata nyayo za Lloris na Karim Benzema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live