Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Varane achefua watu Ufaransa

Raphael Varane Pic Raphael Varane

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Raphael Varane amepondwa baada ya kutangaza amestaafu kucheza soka la kimataifa na mkongwe aliyewahi kuichezea timu ya taifa Ufaransa, Jerome Rothen akidai ni upuuzi mtupu.

Mkongwe huyo aliicheza Ufaransa mechi 13 anaamini ndani ya miaka minne aliyochezea timu ya taifa Ufaransa, anaamini Varane amefanya maamuzi mabovu.

Varane amestaafu kucheza soka la kimataifa na akili yake imejikita zaidi kwenye soka la ngazi ya klabu akiwa na kikosi cha Manchester United.

Beki huyo alikuwa na mchango mkubwa akiisaidia Ufaransa kubeba Kombe la Dunia katika fainali zilizofanyika Russia mwaka 2018, katika fainali zilizofanyika Qatar mwaka huu Ufaransa iliangukia mbele ya Argentina kweny mechi ya fainali.

Sasa mashabiki na wakongwe waliowahi kukipiga katika timu ya taifa Ufaransa wamechukizwa na maamuzi yake ya kustaafu, kwani wanaamini bado ana nafasi ndani ya kikosi kuelekea michuano ya EURO itakayoanza mwakani.

"Umri wake bado unaruhusu ana uwezo wa kucheza soka la daraja juu, ukifikia umri wa miaka 29, majukumu ya kuibeba timu ya taifa yanakuwa makubwa, unatakiwa uonyeshe ubora wako kwaajili ya taifa lako, nimeshangaa sana sijaona sababu, sijaona mchezaji wa Ufaransa aliyestaafu soka akiwa na umri wa miaka 29, tunafahami alikuwa na mchango mkubwa lakini kwenye hili amezingua," alisema mkongwe huyo.

Chanzo: Mwanaspoti